0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jan 20, 2013

TRISH ZEMBA: JE NI MUUJIZA GANI ULIMTOKEA BINTI HUYU....?


Trish Zemba

Desemba 24, 1993, siku moja kabla ya sikukuu ya Krismas, msichana Trish Zemba alipanda farasi akiwa anataka kwenda kutembea, pengine kuwaalika wenzake kwa ajili ya sikukuu ya Krismas au kwa sababu nyingine. Akiwa njiani, farasi wake alibadilika na kuanza kufanya vitimbwi, ambapo hatimaye alimwangusha chini msichana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 14 wakati huo.

Trish aliumia mguu, ingawa siyo sana. Alilazimika kurejea nyumbani akiwa na maumivu. Baada ya huduma ya kwanza, alipata nafuu kubwa na haikuonekana kama alikuwa ameumia asubuhi ya siku ile. Kwa hiyo alisherehekea Krismas yake vizuri tu. Lakini siku kumi baadaye akiwa bafuni asubuhi alipoteza fahamu na kuanguka. Kuanguka huko kulimtonesha mguu mahali alipokuwa ameumia wakati wa ajali ya farasi. Ilibidi apelekwe hospitalini ambako alilazwa.

Madaktari walihangaika kutafuta sababu ya chanzo cha tatizo lile bila mafanikio. Lakini, hatimaye walibaini kwamba, msichana yule alikuwa na tatizo ambalo huwapata watu wachache sana hapa duniani, linalofahamika kitaalamu kama Reflex Sympathetic Dystrophy (RSD). Ukweli ni kwamba, tatizo hili huwa halina tiba zaidi ya ile ya kukata kiungo kilichoathirika. 

Ni tatizo lenye kusababisha maumivu makali sana kwa mgonjwa na kuoza kwa kiungo kilichohusika. Pamoja na madaktari kutumia zile dawa kali kabisa ambazo zinakaribia kuwa kama sumu kwa ukali, bado Trish alikuwa akihisi maumivu makali. Maradhi haya yana tatizo la kumfanya mtu kuhisi maumivu makali kupita kiasi, hata kama ameumia kwa kujikwaruza tu.

Pamoja na yote hayo, wazazi wa Trish walikuwa wakisema kwamba, haitakuwa rahisi kwao kupoteza imani kwamba, mtoto wao amepona. Walisali na kuomba, na kubwa zaidi, waliamini kwamba, binti huyo mdogo angepona tu, bila kujali anaumwa kitu gani au kwa kiasi gani.

Asubuhi mchana na jioni walikaa wakiomba ili binti yao aondokewe na maumivu. Kila mmoja moyoni mwake, alikuwa akiamini kwamba, nguvu fulani itafanya kile wanachokiomba, yaani binti yao kuachwa na maumivu yale. Wakati hilo likiendelea madaktari waliamua kwamba, ni vyema kwao kumkata mguu binti yule ili kumnusuru na adha ile. 

Wenyewe waliamini kwamba, mguu ukikatwa, maumivu yatakwisha na hivyo itakuwa rahisi kwao kushughulikia kidonda. Wazazi walikubali, ingawa bado walikuwa wanaamini kwamba, binti yao angepona bila kukatwa kiungo. Kwa nini walikuwa bado wakiamini vile? Ni wazi ni kutokana na imani kubwa waliyokuwa nayo kwa Mungu au chochote wanachokiamini.

Ilibidi wasaini kwamba, binti yao akatwe mguu. Hata hivyo waliaendelea kuomba na kujiambia kwamba, kila kitu kitabadilika ghafla. Kwani kuna nguvu kubwa zaidi. Asubuhi walikwenda hospitalini kumwona binti yao, ikiwa pia ni kushiriki kwa njia moja au nyingine kumpa moyo kuhusiana na kukatwa mguu.

Hii ilikuwa ni subuhi ya Machi 11, 1994, pale ambapo wazazi walipofika kwenye chumba cha binti yao, waliogopa sana walipomwona akiwa amesimama. Ukweli ni kwamba, kwa maumivu yake hata kukaa ilikuwa ni vigumu, achilia mbali kusimama. Ilibidi wazazi wale waamini, lakini walishikwa na hofu pia ya uwezo wa imani zao wenyewe.

Trish mwenyewe alipohojiwa alisema, asubuhi sana ya siku ile ambayo ndiyo ilikuwa akatwe mguu , alihisi maumivu yakishuka kutoka mapajani na kwenda chini miguuni na halafu yakawa hayapo. Alijaribu kuinuka na alijikuta akimudu. Kwa muda wa zaidi ya miezi miwili na nusu, hakuweza kukaa angalau kwa zaidi ya sekunde moja bila maumivu, lakini baada ya uponyaji wa miujiza aliweza kusimama.

Je mnasemaje kuhusu jambo hili……?
This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi