0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Oct 10, 2009

NJIA YA MAISHA YAKO INAPOFUNGWA GHAFLA!

Ni kidonda kikubwa cha hisia, lakini nimemudu kukiponyesha na sasa limebaki kovu tu ambalo halina mauamivu kwangu. Kidonda hiki cha kihisia kilitokana na mkwaruzo ulioanzia kwenya familia yetu, yaani kwa wazazi wangu. Ndoa ya wazazi wangu haikuwa ndoa imara na wala mtu asingepaswa kuiita ndoa.

Nilizaliwa mwaka 1965 katiaka kijiji cha Segera, mkoani Tanga, kabla ya wazazi wetu hawajahamia Sindeni wilayani Handeni wakati huo, ambako ndiko nyumbani kwa baba yetu. Mama yetu alikuwa anatokea maeneo ya Mombo mkoani Tanga. Tulizaliwa wawili tu kwa baba na mama, mimi na mdogo wangu wa kike.

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi