0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jul 10, 2009

NI MAREHEMU KATIKA MWILI MWINGINE?

Hivi huyu nishamuona wapi?

Kuna wakati unakuwa mahali, halafu unahisi kwamba ulishakuwa mahali hapo kabla, na pengine ukiwa na watu wale wale. Lakini, kwa unavjojua, hujawahi kuwepo hapo, wala kuwa na kuwa na watu hao.

Hali ya uzoefu huu kufahamika kitaalamu kama Déjà vu. Kama nilivyosema awali kwamba, unakuwa katika sehemu ngeni unashangaa kuona kama kwamba, ulishawahi kwenda sehemu hiyo huko nyuma.

Unaona na mtu kwa mara ya kwanza lakini unapata mawazo kama uliwahi kuonana naye huko nyuma. Hiyo ndiyo Déjà vu.

Neno Déjà vu, asili yake ni lugha ya kifaransa ikiwa na maana kwamba, Tayari nilishawahi kumuona au mahali hapa niliwahi kupaona kabla, ikiwa na maana kwamba mtu anakutana na kitu kipya katika mazingira mapya na anagundua kwamba aliwahi kukumbana na hicho kitu kabla, pengine katika mazingira hayo hayo.

Inasemekana kwamba, mambo haya ya Déjà vu ni ya kawaida. Kila watu saba katika kial kumi wanasema kwamba waliwahi kuukumbana nayo angalau mara moja katika maisha yao.

Neno hili Déjà vu lilitumiwa kwa mara ya kwanza na Emile Boirac (1851-1917), ambaye alikuwa mtafiti wa Kifaransa wa mambo ya akili za ziada za watu. Kuna maelezo mengi ya uzoefu huu, kama ifuatavyo: Unakutana napicha kwa mara ya kwanza lakini unagundua kwamba uliwahi kuiona zamani.

Unafika mahali pageni na unagundua kwamba, mahali pale si pageni bali uliwahi kufika kabla. Lakini, kwa akili ya kawaida, unakumbuka kwamba hujwahi kufika hapo. Unaiona sinema mpya lakini unahisi kwamba uliwahi kuiona kabla. Na cha kushangaza ni kwamba unaweza hata kutabiri kitendo kitakachofuata na ikawa kweli, lakini hukumbuki na pengine hujawahi kuiona, kwani ni sinema mpya.

Unakumbana na hali fulani au unafika mahali fulani pageni lakini unagundua kwamba hali ile au mahali pale uliwahi kupaona katika ndoto zako huko nyuma.
Déjà vu pia inaweza ikaonekana katika unusaji, ladha ya chakula, mchanganyiko wa rangi, sauti ya juu au ya chini, kelele au kitu chochote ambacho kinafukua kumbukumbu ya mambo ya zamani.

Mtu mgeni aliye mmbele yako uvaaji wake na namna anavyoongea anaweza kukukumbusha mtu uliyekuwa umekutana naye kabla. Baadhi ya watu wanasema kwamba hali hii ya kufanana inaweza kusababishwa na hali ya ubongo kwa wakati huo.

Watu wanaamini kwamba binadamu baada ya kufa roho yake inaingia katika mwili wa mwingine, wanasema kwamba kwa mujibu wa Déjà vu waliwahi kukumbana na hali kama hiyo zamani. Kunaweza kukawa na sababu na maelezo chungu nzima kuhusu Déjà vu.
This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi