0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Mar 15, 2009

TUNAJIDANGANYA KWA KUAMINI KUWA NDOA NI TENDO!

Hakuna haja ya kununiana

Baadhi yetu tumelelewa na kukutana na mazingira yaliyotufundisha hivyo kwa hiyo ndivyo tunavyoamini. Tunaamini kwamba tunapooa au kuolewa tunafanya hivyo ili kushiriki tendo la ndoa kama dhana ya kwanza. Ni kitu gani kinachotokea basi pale ambapo haturidhiki na kuridhishwa kiunyumba na wake au waume zetu? Ni kwamba huwa tunadhani au kuamini kwamba hapo ndoa haina maana na hivyo huwajengea chuki wenzetu na pengine kutoka nje ya ndoa zetu tukidhani tutapata nafuu.

Hebu tujiulize je ni kweli dhana ya ndoa ni kufanya mapenzi? Jibu ni siyo kweli hata kidogo. Hebu tujiulize tena baada ya kuoana na kuishi kwenye ndoa kwa muda fulani wake au waume zetu wakapata matatizo ya kimaradhi au ajali au mengine ambayo yatawafanya wasiweze kabisa kushiriki jambo hili tutafanyaje? Huenda jibu kwa wale wanaoamini kwamba ndoa maana yake ni kufanya mapenzi watasema kwamba watakwenda nje au kwa wanaume wataoa wake wengine. Huu ni ujinga mkubwa mno kwani tunaweza kufanya hivyo ikiwa ni wenzetu waliopata matatizo lakini kama ni sisi tutaona inavyoumiza.

Tendo la ndoa katika ndoa ni muhimu na kwa kiasi cha kutosha husaidia pia kuimarisha uhusiano. Lakini pale kunapokuwa na tatizo kwenye suala hilo ndipo hapo upendo unapopimwa kama ni wa dhati, bandia, au upendo wa kimradi. Kama upendo wetu ni wa dhati tutajitahidi kuangalia mazingira ambayo huenda yatawafanya hao wenzetu wawe kama walivyo. Tunapojadili kwa upendo udhaifu fulani ni wazi tutawapa wengine nguvu ya kujikagua na kuzidisha upendo kwetu.

Lakini tunapokuwa wakali na kulaumu au kuchukia na kulaani tutawafanya wenzetu wajione wanyonge na pia tutawafanya au kuwapa nafasi ya kuhalalisha kwamba huenda sisi tumetawaliwa sana na tamaa ya kimwili kuliko uwezo wa kufikiri kiasi kwamba linapotokea tatizo tunakuwa vichaa na hivyo uwezekano wa kutoka nje au kuvuruga ndoa ni mkubwa. tujifunze kufahamu na kukubali ukweli kwamba ndoa bora na imara hazifanywi hivyo na tendo la ndoa, bali hufanywa hivyo na wanandoa kusaidia kutatua kila tatizo linalotokea.

Ni vizuri tukawa wazi kusema matatizo tunayohisi kwa wenzetu badala ya kuhisi tu na kudhani watayaona. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeshindwa jukumu letu la kupenda kwani tutakuwa tumejitazama wenyewe zaidi..
This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi