0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Mar 13, 2009

KAMA KIFO HUJA HIVI, BASI KIFO NI KITAMU.

Sioni sababu ya kukihofia kifo tena

Nilikuwa nimelala sebuleni kwenye mkeka huku nikiwa nimelalia mto, ni wakati huo ndipo nilipoanza kuhisi visindano vikinichoma kwenye nyayo, lakini havikuwa na maumivu sana.

Ghafla nilianza kuhisi miguu ikianza kufa ganzi na kupoteza uhai taratibu, na kwa kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kwenda ndivyo ile ganzi ilivyokuwa ikizidi kupanda. Ile hali iliendelea hivyo hadi mpaka kwenye nyonga, na kutoka kwenye nyonga ghafla ilipanda mpaka shingoni, hadi hapo nilihisi kama kuna jambo ambalo si la kawaida linanitokea kwani mwili wangu kuanzia miguuni mpaka shingoni ulikufa kabisa, yaani nilihisi kama nimekatwa shingo na kubakia na kichwa tu chenye uhai, nilianza kupaza sauti kumuita mama ambaye alikuwa jikoni akiendelea kuandaa chakula cha jioni.

Nilimsikia mama akinijibu kwa mbali kuwa anakuja lakini sikuoana dalili ya yeye kuja, mara mdogo wangu wa kiume akapita pale sebuleni na kuniona, kwa kweli sijui alihisi nini kwani nilimsikia akipiga kelele za kumuita mama huku akisema “ Mama Eggy anakufa”
Mama alikuja mbio ,alipofika na kuniona nae alipiga kelele “mama yangu mwanangu anakufa”

Kuanzia hapo sikujua kilichoendela, lakini katika hali ya kustaajabisha nilijikuta nikiwa nautazama mwili wangu ukiwa umelazwa kitandani hopitalini, na hospitali yenyewe nilikuwa naifahamu vizuri kwani ilikuwa iko jirani na nyumbani. Sijui hasa nilikuwa nimekaa au nimesimama, nilikuwa kama naelea hewani lakini nilikuwa nauona mwili wangu umelala kitandani nikiwa nimetoka humo.

Nilimuona daktari ambaye nilikuwa namfahamu alikuwa amesimama akiendelea kuchukuwa vipimo, na pembeni alisimama nesi mama mtu mzima akiwa anaruka ruka kwa wasiwasi kwa kuchanganyikiwa huku akisema “Daktari angalia asije akatufia hapa mtoto wa watu” yule daktari hakumjibu aliendelea kuufanyia mwili wangu vipimo lakini jasho lilikuwa likimtoka hasa nadhani ni kwa ajili ya wasiwasi, baada yakipimo cha mapigo ya moyo kutompa majibu aliyoyategemea.

Mwili wangu ulikuwa umevaa gauni la bluu ambalo nilihisi hilo gauni lilikuwa ndio tatizo hivyo nilipata wazo la kwenda nyumbani ili kuchukuwa nguo lenye rangi nyingine ili niweze kubadilisha na kutoa lile gauni.

Kabla sijaenda nyumbani kuchukuwa nguo, nilitoka nje ya chumba kilichokuwa na mwili wangu, na kuwaangalia mama na kaka yangu ambao walikuwa wamekaa kwenye korido ya ile hospitali, walikuwa wanalia wakidhani kuwa huenda nitakufa. Niliwatoa wasiwasi kwa kuwaambia kuwa wasilie kwani mimi ni mzima, lakini hawakunisikia na wala hawakuonesha kwamba walikuwa wakiniona pamoja na kwamba niliwasogelea karibu.

Niliondoka pale na mwendo wangu ulikuwa ni kama upepo kwa kuwa huo mwili niliokuwa nao ambao ndio mimi hauwezi kujibainisha kama huu mwili tulio nao, ingawa nilikuwa na ufahamu wa kila kitu na kila jambo lililokuwa liliendelea kwa wakati huo.
Niliweza kupenya ukutani na darini kwa staili ya kuelea, na nilipofika nyumbani nilifungua kabati langu ili kuchagua gauni lingine, lakini sikupata gauni nililolitaka, hivyo niliamua kurejea kule hospitalini.
Nilipofika nilimkuta yule daktari akiwa bado amekaa na kushika tama na yule nesi alikuwa analia huku akisema “ masikini mtoto wa watu”

Nilianza kuukagua mwili wangu tena, ghafla ukatokea ukimya wa ajabu, kama vile nilikuwa nasubiriwa kufanya uamuzi, nikajiambia “ pengine haya yamenikuta kwa kuwa simjui mungu” nilijikuta nikisema kwa sauti ambayo hata hivyo haikuwasitua waliokuwa pale ndani “Mungu usiniuwe hadi nikujue”

Itaendelea wiki ijayo………….
This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi