0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Dec 29, 2008

JE, MWANAMKE/MWANAUME KUFUJWA KATIKA UHUSIANO NI KUTOKUJIAMINI AU KUOGOPA KUACHWA?

Imesemwa sana na itaendelea kusemwa kuhusu kutojiamini kwenye uhusiano. Wataalamu wanaamini kwamba, watu wasiojiamini, wanakuwa na matatizo makubwa na magumu au mabaya zaidi wanapokuwa kwenye uhusiano, kuliko kwenye maeneo mengine ya kimaisha.

Kwa wanawake wanakabiliwa na adhabu mbili kwenye jambo hili. Kutokana na mfumo dume, mwanamke anakuwa tayari amepoteza kujiamini anapokuwa mbele ya mwanamume. Wakati mwingine hata kama alikuwa akijiamini hapo kabla, yaani kabla hajaingia kwenye uhusiano.

Kwenye uhusiano wa kifujaji, kama mwanamume ndiye mfujaji, mara nyingi sana, mwanamke aliye kwenye uhusiano huo, anakuwa ni yule mwenye kupenda kujibandikiza kama kupe, ambaye anaamini kuwa hawezi kuishi bila mume huyo. Anapigwa, analaliwa nje, anadhalilishwa kwa njia mbalimbali, lakini ameng’ang’ania.

Ni mara chache sana kukuta mwanamke asiye na utegemezi, yaani asiye tayari kumng’ang’ania mtu, kuolewa na mume mnyanyasaji. Kwa kuwa mtegemezi, mwanamke hatimaye humaliziwa kujiamini kwake kote.

Umewahi kukutana na mwanamke ambaye amewahi kuwa na msululu wa wanaume wanyanyasaji? Anaishia kubadili kutoka kwa mnyanyasaji wa kwanza, wa pili na kwendelea. Hajui kwamba, anakutana na wanaume hawa kwa sababu ya kutojiamini kwake.

Mwanamke anayejiamini hana hofu ya kumwacha mwanamume mnyanyasaji. Anajua kwamba hastahili kufanyiwa vile. Anatengeneza nguvu ya kihisia yake mwenyewe na anakuwa barabara, ngangari hata akiwa peke yake.
Mvuto wa kimapenzi ni nguvu kubwa sana, kama inavyojidhihirisha katika wingi wa picha za wanawake waliokaa kihasara hasara katika magazeti mengi. Wanaume hasahasa, wanaathiriwa sana na wanawake warembo. Baadhi ya wanawake wanagundua kwamba wanaweza kuwasisimua wanaume kwa kukaa au kuvaa kihasara hasara.

Mwanamke asiyejiamini ambaye anataka kibali cha kujihakikishia kuwa yeye ni mzuri au la toka kwa wengine, hutegemea mvuto wa kimapenzi kama ‘gia’ yake ya kuonekana.

Mwanamke anayejiamini hahitaji kukubalika kwa wengine kama ni ajenda yake ya kila siku.
Anajiamini kiasi cha kuweza kujidhihirisha katika uwezo wa aina nyingi; si katika kutegemea mvuto wa kimapenzi pekee.
Katika fasihi nyingi nilizosoma, karibu zote zinasisitiza umuhimu wa kujitegemea kabla ya kuingia katika uhusiano wowote.

Kama ningeweza kutoa ushauri wa kitabu cha kusoma ili mtu awe salama zaidi, ningeshauri kila mtu asome kitabu cha cha Stephen Covey.
Anazungumzia kufanikisha kujishinda mwenyewe kabla ya kuwashinda wengine.
Anazungumzia kuhusu mchakato toka kuwa mtu unayetegemea, unayejitegemea na unayetegemeana na wengine.

Kutojiamini au kuhisi kuwa huko salama hadi wengine wawepo au wathibitishe, kunaweza kusababisha madhara makubwa, hasa kama hujui kutojiamini maana yake nini. Watu wengi wasiojiamini wanapenda kutoa visingizio wanapopata matatizo, wakiwa hawajui kwamba wao wenyewe ndiyo chimbuko la matatizo waliyo nayo.

Mwanzo wa kuwa salama ni kujifunza kujicheka, ukijua kwamba hakuna mtu asiyekosea!
Jiambie kwamba, umekamilika na usitake mume au mke akukamilishe, kwani hataweza.

Jipende mwenyewe kwanza.


This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi