0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Dec 26, 2008

MWANZO WA BINADAMU. BADO NATAFUTA MAJIBU........

Bado naendelea kupata changamoto, awali nilitaka niachane na hii mada kwa sababu kwa jinsi ninavyozidi kutafuta majibu ndivyo ninavyozidi kupata maswali mengine.

Haya sasa, Rafiki yangu Bwaya naye kaja na changamoto nyingine.


Hapa inabidi nitulie kidogo.

Ukweli ni kwamba namuheshimu sana huyu bwana, kwani mjadala huu niliuanzisha kutokana na makala zake ambazo kama mnakumbuka niliwahi kuziunganisha katika makala yangu ya kwanza wakati naanzisha mjadala huu.

Wako baadhi ya wasomaji wangu ambao hawakunielewa kwa kudhani kuwa napinga hoja za bwana Bwaya, labda niweke wazi kwamba sikuwa na msimamo unaotofautiana sana na yeye, bali lengo langu lilikuwa ni kujaribu kuhoji baadhi ya nadharia ambazo bado zilikuwa zinaacha maswali.

Hata hivyo, sikatai kama zipo hoja ambazo zilikuwa zinaonyesha kutofautiana na yeye, naamini hiyo ilikuwa ni changamoto nyingine katika kujaribu kuibua hoja mpya.

Lakini kama alivyowahi kusema bwana huyu kwamba hakuna kujifunza bila ya kutofautiana, nadhani tofauti hiyo imeleta mwanzo mpya wa mjadala huu.

Ukweli ni kwamba nisingependa kuufunga kabisa huu mjadala ili tuwape nafasi wanazuoni watarajiwa ambao bado wanaendelea kukaririshwa ujinga huu wa wanasayansi.

Wachangiaji wengine kama Kamala, kaka Kitururu, na dada Yasinta nayaheshimu sana maoni yao, kwani kwa upande wao nao wamesema kile wanachokiamini, bila kuwasahau Mtwiba, na kaka Fadhy Mtanga walioomba nafasi ya kutafakari kabla ya kuleta chanagamoto zao.
Ningependa kuwaambia kwamba mada hii bado ipo na itaendelea kuwepo, nasubuiri changamoto zao waziweke hapa barazani tuzione.

Bwaya kajenga hoja mpya, katika changamoto yake amesema kwamba nadharia ya mabadiliko ipo na mwanaadamu anaendelea kubadilika. Naweza kukubaliana nae.


Lakini, si kwamba mabadilikon hayo yanatokana na uharibifu wa mazingira wa vyanzo vya maji, hewa tunayovuta vyakula vya viwandani tunavokula, madawa ya hospitali tunayotumia kila tuuguapo na kila uchafu uliojaa hapa duniani?

Kwa mfano siku hizi wanazaliwa watoto wenye mapungufu mengi ya viungo, na hata wale wanaozaliwa wakiwa na viungo vyote, bado si salama kwani hukumbwa na mabadiliko mengine kila wanavyokua. Je mabadiliko anayosema Bwaya ni haya au mengine? Hiyo ni changamoto nyingine.

Bado natafuta majibu.

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi